Mgeni rasmi ambaye alipata nafasi ya kufanya
mahojiano ni Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paul Makonda ambaye vyombo vya habari vilikuwa na headlines nyingi kuhusu yeye tangu siku ambayo alitangazwa kuwa DC mpya wa Wilaya hiyo.
Cha kwanza kukizungumzia ni historia ya maisha yake; “Nina
miaka miwili nimekaa Sinza lakini nimekaa Survey miaka miwili.. kwa
hiyo nina miaka minne.. Nilikuwa natoka naenda Chuo na kurudi Dar..”
“Mama
yangu ndio msomi kuliko wote nyumbani kwetu, darasa la saba halafu mzee
hakufanikiwa kuanza hata darasa la kwanza.. Nimepita kwenye mfumo ambao
ulinilazimisha kuwa kiongozi wa maisha ya kwangu mwenyewe, sikuwahi
kufikiri kumfikiria mtu kuamua kwa niaba yangu..”
Safari yake kuwa kiongozi ilianzia huku; “Ndiye
niliyefanikiwa kuwa Rais wa Serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vyote
Tanzania mwaka 2011-12.. Moja nilisaidia kutokomeza mgogoro wa mgomo
uliokuwa unasababishwa na Bodi ya Mikopo.. Nilifanya kazi ya
kushirikisha Bodi ya Mikopo ikubali kuajiri Watumishi wa Bodi ya Mikopo
kwa kila Chuo. Pili kulikuwa na shida ya kuhama, tukafanikiwa
kutengeneza mfumo ukiwa unasoma accounts Arusha ukahama na accounts yako
mwaka wako ukaja ukaendelea na IFM darasa lilelile na mwisho
ukamaliza..”
Hapa anazungumzia ishu ya kupingwa na watu wengi baada ya kuteuliwa; “Huo
ndio uhai wa fikra, haiwezekani watu wote waunge mkono mambo yote..
Kupingwa kunakufanya wewe uwe kiongozi imara.. ni utamaduni wa kawaida
watu kukataa mambo wasiyoweza kuyaona, tuna tabia ya kukubali kitu baada
ya kitu hicho kuwa kimeondoka. Haiwezekani wananchi hawakusemi halafu
unataka kuwaongoza”
Kuhusu tukio lililoandikwa na Magazeti kwamba alimfanyia vurugu Mzee Warioba; “Tukio
lile halijaathiri chochote, limeongeza thamani yangu katika jamii..
Mtu mwingine anaweza akasema hii mbona inaenda kumzamisha kwangu mimi
najua ni sehemu mojawapo ya kunisaidia mimi kwenda hatua moja kubwa..”
“Kilichosemwa
sicho chenyewe matokeo yake kimenisaidia kunizalishia marafiki
kunikaribishia marafiki wengi kuliko maadui.. kila akisema Mzee Warioba hakuna anayeandika mwisho wa siku huwa namwambia mzee wewe kaa kimya.. Inafika kipindi nasema labda kuna Mzee Warioba mwingine, kama Mzee Warioba anasema sivyo lakini kuna watu bado wanaandika maana yake kuna Warioba mwingine ambaye Makonda hamfahamu na Mzee Warioba naye hamfahamu”
Mipango ya Makonda kwenye Wilaya ya Kinondoni; “Leo
ni siku yangu ya tatu.. nimejipa muda ndani ya siku 90 naamini
Kinondoni itakuwa tofauti na jinsi ambavyo watu wanavyoitazama“