Ni
zaidi ya mara tatu kumekuwa na mijadala ndani ya Bunge la Tanzania
tumesikia ikijadilia kuhusu njia ambayo inhesaidia kutafuta suluhu ya
kudumu kwenye ishu ya tatizo la wanafunzi shule za Msingi na Sekondari
kupata ujauzito.
Leo nimekutana na hii story nikajua
kwamba kumbe tatizo hili sio la Bongo peke yake, Indonesia wao wameenda
mbali zaidi, Jimbo la Java Mbunge mmoja alitoa pendekezo la kuwa na
utaratibu wa kuwapima wanafunzi wa kike wanaomaliza shule za Sekondari
kama wamewahi kukutana kimwili na wanaume, iwapo yoyote anakutwa kwenye
hali kwamba aliwahi kukutana na mwanaume basi safari yake kimasomo
itaishia hapo hatoruhusiwa kuendelea na masomo.
Ni nchi hiyo hiyo mwaka jana ilitoka
ripoti ya utafiti iliyosema kumekuwa na zoezi la kupima hivyo askari wa
kike na wanajeshi kitu ambacho kilikosolewa na watu wa haki za binadamu.
Viongozi wa dini pia walilaumu hilo japo
walisema kuna dalili zote kwamba ishu hiyo imeendelea kufanywa chini
chini kwa siri japo Serikali ilisisitiza kwamba haitoruhusu utaratibu
huu kuwepo katika nchi hiyo.