Mhubiri mmoja huko Brazil, Alex Novais de Brito
aliyekuwa akifanya mahubiri kwenye mazishi ya muumini wake amejikuta
akishindwa kumaliza ibada hiyo baada ya udongo wa kaburi kudidimia na
kufanya Mchungaji huyo na waumini wengine watatu kudumbukia kwenye
kaburi.
Hilo lilitokea kwenye makaburi ya Campo da Esperanca wakati kukifanyika ibada ya mazishi.
Watu wawili walipelekwa Hospitali ya
jirani ili kutibiwa majeraha madogo waliyoyapata baada ya kuanguka, watu
walichanganyikiwa baada ya kutokea tukio hilo, Mhubiri huyo alijikuta
kwenye wakati mgumu na kushindwa kumalizia ibada.