Hali ya mama mzazi wa mtoto albino Aliyekutwa kafukiwa shambani huko GEITA hairidhishi

Hali ya ESTHER JONAS, ambaye ni mama mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyetekwa na kufariki Dunia baada ya kukatwa viungo, imeelezwa na madaktari wa hospitali ya rufaa BUGANDO alikolazwa kuwa ni mbaya baada ya kushindwa kupumua kutokana na kuvimba sehemu kubwa ya mwili ikiwamo kichwani.

Mama huyo ESTER JONAS, mwenye umri wa miaka 30 ambaye jana amefanyiwa upasuaji wa kichwa katika hospitali ya rufaa ya BUGANDO imebadilika ghafla usiku wa kuamkia leo na madaktari wamemuwekea mipira puani kwa ajili ya kumsaidia kupumua ili kuokoa maisha yake.
 
Mkuu wa kitengo cha dharura katika hospitali ya BUGANDO DK. DERICK DAVID amesema kuwa hali ya mama huyo sio nzuri na kwamba kwa sasa anapumua kwa shida na pia hazungumzi na kuongeza kuwa kinachofanyika sasa ni kuendelea kumsafisha vidonda na kumpa antibaotiki ya kukausha vidonda.
 
Mwenyekiti wa chama cha walemavu wa ngozi mkoani mwanza ALFRED KAPOLE ametoa tamko kuhusiana na tukio hilo.
 
Mwanamke huyo mkazi wa kijiji cha Ilelema wilayani Chato mkoani Geita alishambuliwa na watu wasiojulikana na kisha kuporwa mtoto wake mwenye ulemavu wa ngozi – albino aitwaye YOHANA BAHATI mwenye umri wa mwaka mmoja aliyekuwa Amebebwa mgongoni wakati akipika chakula cha usiku.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo