Shule
ya sekondari ya ENDAROFTA iliyoko wilayani karatu inakabiliwa na tatizo
la uhaba wa maji tangu imeanzishwa zaidi ya miaka ishirini sasa hali
inayowalazimu wanafunzi kutumia zaidi ya masaa sita kwa siku kutafuta
huduma hiyo.
Wakizungumza shuleni hapo wanafunzi wa shule hiyo wanasema pamoja
na jitihada zinazofanywa na uongozi wa shule kuwaletea maji kwa
baadhi ya siku bado yamekua hayatoshelezi mahitaji na hivyo kupoteza
muda mwingi wa masomo.
Pamoja na tatizo hilo la maji shule hiyo pia inakabiliwa na
uchakavu wa majengo yakiwemo mabweni ambayo hayawiani na idadi ya
wanafunzi hali ambayo imewasukuma baadhi ya wanafunzi waliosoma shuleni
hapo miaka ya nyuma kuchanga fedha na kukarabati bweni moja pamoja na
kununua vitanda na magodoro kwa lengo la kuboresha mazingira ya usomaji.
Shule hiyo inamilikiwa na kanisa katoliki jimbo la mbulu,mwakilishi
wa askofu wa jimbo hilo FATHER VITALIS MATSEY na wadau wengine wa
elimu wanasema jukumu la kuboresha elimu nchini lipo mikononi mwa
watanzania wenyewe bila kutegemea misaada kutoka nje mfano mzuri ukiwa
kundi hilo la wanafunzi waliosoma shuleni hapo.