MEYA WA ILEMELA AWAPELEKA TAKUKURU WABUNGE WA CHADEMA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Meya anayejiita 'wa Mahakama' wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata amewaburuza TAKUKURU madiwani wanne wa CHADEMA.

Fikra Pevu limebaini madiwani hao, JOSEPHAT MANYERE , ROSE BROWN, GLADYS KIWIA na LUCY KAZUNGU, wanatuhumiwa kupokea posho ya zaidi ya Sh milioni 3 bila kusafiri.

Madiwani hao wanatuhumiwa na Meya kwamba kila mmoja alipokea posho ya ya shilingi 80,000/- kwa siku kumi kila mmoja kwa safari ya kwenda Mbeya kikazi lakini hawakwenda.

Habari za uhakika zilizothibitishwa na maofisa wa Takukuru, Mwanza, taarifa imewasilishwa kwao jana.

Kwa mujibu wa  Meya huyo, madiwani hao wanastahili adhabu kwa mujibu wa Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 329 ya mwaka 2002.

Meya huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangiri alipata udiwani kwa tiketi ya Chadema kabla ya kuvurugana na Chama chake na kamati kuu kuamua kumtimua uanachama na yeye kukimbilia mahakamani kuzuia kutimuliwa, kesi hiyo iko Mahakama kuu inaendelea kuunguruma.

Amekuwa akijiita Meya wa Mahakama kwa kuwa Mahakama ndiyo ilizuia kufukuzwa kwake na hivyo kumfanya aweze kugombea umeya ambao alishinda kwa kuungwa mkono na CCM.

Matata tayari ameshawafukuza udiwani madiwani wawili wa Chadema, Kahungu wa kata ya Kirumba na Abubakari Kapera wa kata ya Nyamanoro kwa kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo wakati wakigomea vikao wakigoma kumtambua yeye kama Meya.

Manyerere ambaye ndiyo alikuwa Meya wa Jiji la Mwanza baada ya uchaguzi Mkuu wa 2010 kabla halijagawanywa kuzaa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza lenyewe, aliondolewa katika kiti hicho kwa zengwe lililoanzishwa na diwani wa Igoma kupitia Chadema Adam Chagulani, na kuungwa mkono na Matata na madiwani we CCM na CUF. 
 
Chagulani  alifukuzwa Chadema kufuatia kuanzisha hoja ya kutokuwa na Imani na Meya wa Chama chake, yeye pia alifungua kesi mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama.

Chanzo:Fikrapevu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo