Mtoto
Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliyepotea tarehe 15 wilayani
chato amepatikana amekufa huku akiwa hana baadhi ya viungo vyake vya
mwili.
Akiongea katika kitongoji cha mapinduzi ndani ya pori la
hifadhi kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Joseph Konyo amesema maiti
ya mtoto huyo iligunduliwa na mpita njia katika shamba la mahindi
lililopo kitongoji cha tatu kutoka nyumbani kwao, baada ya kuona kipande
cha nguo yenye damu ambapo alipiga yowe lililowakusanya wanakijiji
ndipo walifukua shimo alipokuwa kafukiwa na kukutwa akiwa hana mikono na
miguu yote.
Hali ya mama Ester Jonas ambaye ni mama wa mtoto huyo bado ni tete
na madaktari wa hospitali ya rufaa Bugando wanaendelea na juhudi za
kuhakikisha hali yake inaimarika.