Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema yeye ni mtu mwadilifu ambaye hajawi kutoa wala kupokea rushwa kwa mtu katika maisha yake yote.
Pinda amesisitiza kwamba ana hakika kuwa hata siku moja hawezi
kukamatwa kwa kosa la kupokea rushwa,isipokua kuna watu wanamchafua mara
baada ya kutangaza nia yake ya kuvaa viatu vya Rais Kikwete.
Alisema kuwa wako baadhi ya watu walipanga kumchafua kwa kutaka
kumsingizia wakati wa mkutano wa 16 na 17 Bungeni kwamba anahusika na
uchotwaji wa fedha za Escrow.
“Nilishangaa sana watu ambao walitaka kunichafua kwa kunihusisha na
fedha za Escrow,mimi sihusiki na wala sitahusika hata siku moja katika
kupokea na kutoa rushwa mahali popote pale”alisisitiza Pinda.
