Mwanafunzi wa Darasa la pili katika shule ya msingi Ungindoni kata ya
Mji mwema Dar es salaam anadaiwa kuchomwa moto na mama yake mkubwa
sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia jalo.
Mtoto huyo alifanyiwa ukatili huo siku ya krismasi akidaiwa kula
vipande viwili vya nyama na hivyo kupewa adhabu na mama yake huyo kwa
kuchomwa moto kwenye paja,mikono,magoti na miguu.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo alisema majirani walibaini kujeruhiwa
kwa mtoto huyo mara baada ya kutoka nje na kuonekana akichechemea na
alipoulizwa alisema amechomwa na na mama yake huku akionyesha maeneo
alikofanyiwa ukatili huo.
Mama mkubwa Rachel alipoulizwa sababu ya kufanya hivyo alisema
alichukua uamuzi huo baada ya kubaini alikula mboga na alipoulizwa
alikana.
“Nakiri nimekosea kimpiga lakini mara kwa mara nimekua nikimuonya aache tabia ya wizi lakini amekua hasikii”alisema Rachel.
