SIMBA WANNE WALIOTOROKA HIFADHI YA TARANGIRE WAUAWA NA WANANCHI

Simba wanne waliotoka nje ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kuingia eneo la kijiji cha Kibaoni, Manyara wameuawa kwa kuchomwa mikuki na wananchi.

Kijiji hicho kipo hatua chache kutoka ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni mojawapo ya vivutio vya utalii wa Tanzania na mara nyingi wayamapori huzagaa mitaani hasa kipindi cha masika kuepuka majani marefu hifadhini.

Tukio hilo ambalo lilielezwa kuw ani janga kubwa katika sekta ya utalii nchini,lilitokea jana alfajiri hadi saa 6 mchana na mizoga saba ya Simba ilipatikana  huku mmoja akiaminika kufia kwenye vichaka baada ya kukimbia alipojeruhiwa.

Waziri wa Maliasili Lazaro Nyalandu ameziagiza mamlaka zinazohusika kuwasaka na kuwatia mbaroni wahusika kuwaongoza wanakijiji hao kuua Simba hao kinyume na utaratibu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo