
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari mauaji hayo ya kikatili na
kutisha yalitokea juzi saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
Kidavashari alisema, siku hiyo
ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe
Meklina Mussa na ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na
kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.
Alisema watu hao waliodaiwa kuwa
na mapanga waliingia chumbani kwa marehemu na kumlazisha mkewe
ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.
Alisema baada ya mkewe
kujifunika walianza kumchinja marehemu kwa kutumia panga huku mkewe
akiwa anasikia jinsi marehemu akilia kwa uchungu.
Kidavashari alisema baada ya
kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na
kukipika kwenye moto uliokuwa unawaka nje ya nyumba ya marehemu.
Alisema kisha walirudi ndani na
kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu na kuziweka kwenye safuria
jingine kwenye moto na kutokomea kusikojulikana huku viungo hivyo
vikiendelea kuchemka ndani ya safuria hizo.