Mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari ya Keko amejifungua mtoto akiwa ndani ya daladala maeneo ya Mtoni Kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam juzi tarehe 23.
Mwanafunzi
huyo ambaye hakuweza kupatikana jina lake mara moja, anasemekana
alijifungua mtoto huyo bila ridhaa yake wakati akiwa katika harakati za
kuitoa mimba hiyo.
Kwa
mujibu wa vyanzo vya habari, msichana huyo anasemekana alikuwa
amekunywa madawa makali kwa lengo la kuitoa mimba hiyo ambayo anadaiwa
kuificha hadi pale alipoumbuka mchana wa siku hiyo.
Haikuweza kufahamika mara moja alikopelekwa mtoto huyo baada ya tukio hilo wala hatua alizochukuliwa binti huyo.