Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Iramba Singida, Halima Mpita amenusurika kifo baada ya kulipukiwa na kitu ambacho kinadhaniwa kuwa bomu la kutengenezwa kienyeji.
Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sidoyeka
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nyumbani kwa Mkurugenzi huyo
wakati akijiandaa kwenda kazini, mlipuko huo ulitoka kwenye bahasha
ambayo aliipokea juzi kutoka kwa Katibu Muhtasi wake.
Ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na ujumbe “Poleni sana, hatuwezi kufanya dili la milioni 90 halafu mkala peke yenu, sisi mkatudhulumu tukawaacha”, baada ya kuisoma alienda nayo nyumbani bila kujua kama kuna kitu kingine ndani.
Wakati akijiandaa kwenda kazini siku ya
jana ndipo mlipuko huo ulipotokea, hakuna aliyekamatwa ila Polisi
wanaendelea na upelelezi wakishirikiana na JWTZ ili kubaini kama mlipuko
huo ulitokana na bomu.
