KILIO TENA: NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA, DAR


Nyumba iliyoteketea kwa moto.
Mashuhuda wa tukio wakitazama nyumba iliyoungua.
Mmoja wa wanafamilia wa nyumba hiyo, Abdallah Mohamed akiwa katikati ya vyumba vilivyoungua.
Baadhi ya vitu vilivyookolewa vikiwa nje ya nyumba hiyo.

NYUMBA moja iliyopo maeneo ya Mwananyamala ‘B’ shuleni,  mali ya Bi. Zena Abdallah imeteketea kwa moto jioni hii. 

Hili ni tukio la pili la moto kuunguza nyumba siku ya leo jijini Dar es salaam baada ya moto mwingine kuteketeza Club Olympia mapema JANA!

Chanzo cha kuungua moto nyumba hiyo inadaiwa ni hitilafu ya umeme uliokuwa ukikatika na kuzima. Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamedai kuwa huenda hitilafu hiyo imetokana na matengenezo ya Tanesco yaliyokuwa yakiendelea kwani chanzo cha hitilafu hiyo  kilianzia upande wa  mita ya umeme  wa nyumba hiyo.

(HABARI/PICHA:  DENIS MTIMA/GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo