Mgogoro umeibuka kati ya watendaji wa manispaa ya Ubungo na kampuni ya kukamata magari yaliyoegeshwa hovyo baada ya wafanyakazi sita wa kampuni ya hepautwa iliyodai kuwa ina mkataba na manispaa ya kinondoni kukamatwa kutokana na kukamata magari ya watu kiholela wakati manispaa ya Ubungo haina utaratibu huo.
Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Sinza Bw Mohamed Fungo amesema wamefanikiwa kuwakamata baada ya kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambao magari yao yamekuwa yakifungwa na kukamatwa ovyo hali iliyowalazimu kuweka mitego huku diwani wa kata hiyo akielezea namna walivyofanikiwa kuwakamata.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Ubungo mbali na kuelezea kero wanayokumbana nayo wamedai kuwa wakati mwingine magari yao wanafungwa wakiwa wameegesha nje ya nyumba zao huku wakiitaka manispaa ya Ubungo kuainisha mipaka yake na kuwatangazia wananchi na makampuni yaliyopewa tenda mbalimbali.
