Ukimya wa askofu Nzigilwa unatokana na sakata la uchotwaji wa zaidi
ya bilioni 300 kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokua katika
benki kuu ya Tanzania BoT.
Alisema kiutaratibu siyo vibaya waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake.
Alisema aliombwa akaunti yake na Rugemarila mwanzoni mwa mwezi
Februari na kwamba hakuwahi kufahamu kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye
akaunti yake hadi alipoangalia taarifa ya benki Februari 27
iliyoonyesha aliingiziwa milioni 40.4.
“Niliwasiliana na Rugemarila na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha
fedha katika akaunti yangu,naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo
anaamini yatasaidia katika shughuli za kitume na
kiuchungaji,,nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa”alisema askofu huyo.