Mbio za urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM zimechukua sura mpya baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kutangaza rasmi kuwania kiti hicho mwakani.
Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapigakura wake Mkoani Singida alisema muda Tanzania kupata maono mapya umefika.
“Muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika,nitachukua hatua ya
kuelekea Dodoma kuchukua fomu muda ukifika,maelfu ya watu
watanisindikiza wanaume,wanawake,vijana kutoka Mikoa mbalimbali.
“Wale wote waliotangaza nia kupitia chama changu kazi zao lazima
zipimwe kwa moto na zianikwe hadharani ili mwisho wa siku CCM yenyewe
itazipima”alisisitiza.
Alisema pindi Rais Kikwete atakapohitimisha utawala wake, lazima atakabidhi kijiti kwa kizazi kipya.
