Aidha alisema huduma ya usafiri wa Reli ya kati,zitaanza mwishoni mwa
mwezi wa Januari hivyo kuwataka wananchi wanaoishi kandokando ya Reli
kuondoka kwani wanahatarisha maisha yao.
“Serikali inawekeza ili tuone tija,na kama tija haionekani basi
uongozi wa juu una shida,hatuwekezi pesa na kunyima sekta nyingine
halafu reli ikabaki vile vile,fanyeni kazi kwa ubunifu la,nitafukuza
wote”alisema Mwakyembe.
“Shirika limejaa mtandao wa wezi tuukiwemo wa mafuta,nimewaonya
iliyopita,kazi yenu wizi tu na kulifanya Shirika likose tija,leo
tunaleta vifaa vya mabilioni ya kodi za wananchi,kichwa kimoja cha treni
kinagharimu bilioni 7,halafu kinapinduka kwa uzembe uzembe tu”alisema.