Waliokua wafanyakazi wa Shirika la ndege ATCL
wamefungua madai ya kuomba kukazia hukumu katika mahakama kuu ya
Tanzania kitengo cha Kazi,wakiomba kukamata na kuliuza jengo la ATC
House ili wafidie malimbikizo ya mishahara yao.
Kwa mujibu wa madai hayo namba 385 ya mwaka 2014 kupitia wakili wao
Benjamini mwakagamba,pia waliomba mahakama hiyo kuteua dalali
atakayeliuza jengo hilo lililopo eneola Posta.
Mmoja wa wafanyakazi hao kapteni Suel Mjungu alisema anadai
sh.72,757,042.48 huku mwenzake Msami akidai sh.114,244,807.3 ambazoni
za awamu ya kwanza walitakiwa kulipwa Oktoba 2013 lakini hadi sasa
hawajalipwa.
