Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Juma Nkamia amenusurika
kupigwa na wananchi jimboni kwake baada ya kutoa kauli zenye kejeli.
Nkamia ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Kusini alikumbwa na hali hiyo
wiki iliyopita alipokua katika kijiji cha Nchemba alipokwenda kuwanadi
wagombea wa CCM katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa
uliofanyika wiki iliyopita.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho alisema Nkamia aliponzwa na kauli za
kejeli alizozitoa dhidi ya aliyekua Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji
hicho Msongozli Yahaya kutoka CUF.
Mkamia alimtuhumu Mwenyekiti huyo kwamba amekua akimchafulia mbele ya
wananchi wake kwa lengo la kumkwamisha katika uchaguzi ujao”Pamoja na
kutoa maneno mengi ya kejeli hali ya hewa ilianza kuchafuka pale ambapo
Nkamia alipoagiza wasaidizi wake wamkamate mwenyekiti huyo aliyekua amekaa
pembeni na kumpeleka katika gari lake.
Baada ya hali hiyo wananachi walianza kuzunguka gari la Nkamia huku
wakiwa na mawe ili kuhakikisha Mwenyekiti wao hakamatwi huku Nkamia
akilizimika kuingia ndani ya gari na kuondoka kwa hofu ya kupigwa.
chanzo:gazeti la mtanzania
