Mwalimu wa chuo cha madrasa kilichopo Chakechake Pemba Said Khamis
ameanza kutumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kutiwa hatiani
kwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 15 jina
linahifadhiwa.
Mwendesha Mashtaka wa Mapinduzi ya Zanzibar Ali Bilal aliiambia
Mahakama mbele ya hakimu kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo miezi mitatu
iliyopita.
Alisema baada ya ucgunguzi wa DNA uliofanywa Tanzania bara ulionyesha
kuwa asilimua 96 mtuhumiwa ndiye aliyempa ujauzito mwanafunzi huyo.
Alisema mtuhumiwa atatumia chuo cha mafunzo jela kwa miaka saba na
atakapotoka atalazimika kulipa fidia ya milioni moja ikiwa ni fundisho
kwa wengine kuacha ufanya vitendo kama hivyo kwa wanafunzi wa vyuo na
madrasa.
