Mahakama
moja nchini Uingereza imenyimwa mwanamume mmoja haki zake za tendo la
ngono baada ya kubainika kuwa mkewe hana akili timamu.
Mahakama nchini Uingereza imemzuia mwanamume mmoja kufanya tendo la ndoa na mke wake ambaye ana matatizo ya kiakili kwa sababu hana uwezo wa kutoa ruhusa kwa mumewe.
Mwanamke
huyo mwenye urmri wa miaka 39 ana ugonjwa wa kiakili wa kiwango cha nne
na saba na ni mke mwenza wa mwanamke wa mke wa kwanza wa mumewe.
Mama
huyo ana watoto wanne na kwa sasa na yuko chini ya uangalizi wa kituo
cha afya kinachowashughulikia wagonjwa wenye matatizo ya akili.
Lakini
jaji aliambiwa aamue iwapo anaweza kurejea kwa mumewe wa miaka 18
ambaye anataka kumwangalia katika nyumba yao ya mjini London.
Mume
huyo anayejulikana kama SA alihoji kwamba ni haki yake kufanya tendo la
ngono na wakeze,iwapo wana akili timamu ya kuweza kukubali na kwamba ni
jukumu lao kukubali.
Alitaka mwanamke huyo kurudi nyumbani ili aweze kutekeleza tendo la ngono na wake zake wawili kwa siku tofauti.
Lakini
Jaji Justice Mostyn ambaye alisema kuwa ndoa ya wake wengi chini ya
sheria ya kiislamu ni halali lakini ni haramu nchini Uingereza aliamuru
kwamba mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina TB hana akili timamu ya kufanya
uamuzi wa kutenda tendo la ngono,na kwamba si vyema yeye kurudi
nyumbani.
Alisema:''Ushahidi unaonyesha wazi kwamba TB hajui tishio la kiafya linalomkabili.
Alishindwa kulinganisha uja uzito na tendo la ngono.
Mwathiriwa hajui vile watoto wake waliovyoingia katika tumbo lake kama anavyoeleza.
Ijapokuwa alifurahia tendo la ngono hakujua kwamba alikuwa na haki ya kuchagua na kukataa.
Kwa
kweli tabia ya SA,kama ilivyo katika utamaduni na dini yake ni kwamba
ana haki ya kutaka kufanya tendo la ngono na wakeze na kwamba wanawake
hao wana jukumu la kukubali''.
Jaji huyo amesema kuwa juhudi za kumuhamasisha TB kuhusu tendo la ngono ,haki zake na hatari iliopo zimefeli.
Aliongezea kuwa TB licha ya kuwa amepata watoto wanne na mke huyo bado angepenbda kufanya tendo la ngono naye.
Maelezo
ya hatua hiyo yamepatikana katika uamuzi uliondikwa na jaji huyo baada
ya kusikilizwa katika mahakama ya utetezi ambayo inatathmini maswala
kadhaa yanayohusiana na watu wagonjwa na wasioweza kujitetea.
Jaji Mostyn alikuwa ametakiwa kufanya uamuzi na shirika la London la Borough of Tower Hamlets linalosimamia maswala ya wanawake.
Mahakama
iliambiwa kuwa wana ndoa hao walikuwa na uhusiano wenye utata na kwamba
kulikuwa na wakati wa ghasia za kinyumbani wakati mume anapokuwa na
hasira.
via>>BBC
