WANAJESHI 54 WA NIGERIA WAHUKUMIWA VIFO KWA KUSHINDWA KUPAMBANA NA BOKO HARAM


Wanajeshi hao wakiwa mbele ya Mahakama ya Kijeshi jijini Abuja nchini Nigeria.

Mahakama ya Kijeshi nchini Nigeria imewahukumu adhabu ya vifo wanajeshi wake 54 waliokataa kupambana na wapiganaji wa Kundi la Boko Haram.

Wanajeshi hao walikutwa na hatia ya uasi, kushambulia na uoga. Wanajeshi hao wanashutumiwa kukataa kupigana kurudisha miji mitatu iliyokuwa ikishikiliwa na Boko Haram mwezi Agosti.

Mwanasheria wa wanajeshi hao amesema wamehukumiwa vifo kwa kupigwa risasi na kikosi maalum huku wanajeshi wengine watano wakiachia.

Vikosi vya Kijeshi vya Nigeria vimedai kuzidiwa silaha na Boko Haram, kwa kuwa hawapatiwi silaha za kutosha kupambana na wanamgambo hao.

Boko Haram wanapambana kuunda himaya ya kiislamu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
CHANZO: BBC


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo