MAKUBWA....KIONGOZI MMOJA MAARUFU AMBAYE ATAGOMBEA URAIS, ETI ATAKUFA MWAKANI 2015

Maalim Hassan Hussein ambaye nimtoto wa aliyekua mtabiri maarufu nchini Sheikh Yahya Hussein ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani,likiwemo la kufariki ghafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenye mbio za kuwania urais mwakani.

Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka gafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali.

Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini pia atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika kutafuta sababu za kifo chake.

Kuhusu uchaguzi Mtabiri huyo alisema kundi la vijana na wazee nyota inaonyesha kwamba watakaofaidika ni vijana lakini kuna wazee pia watakaoweza kufaidika ambao ni wale wenye sura za 'babyface' au wenye kupenda mambo ya ujana.

Alisema ili Tanzania ilinde sifa ya kuwa nchi yenye kuwa na amani na utulivu ni kuwa na rais kijana  mwenye mchanganyiko wa dini mbili au mwenye ndoa ya dini tofauti.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo