Diamond
Platnumz ameingia Dar es salaam Tanzania Dec 02 akiwa na tuzo zake 3
alizozipata kutoka Channel O ambapo Watanzania wamejikusanya barabarani
kutoka Airpot mpaka mitaa aliyokuwa amepita.
Msafara ulipotoka Airpot umepitia Buguruni mpaka Kariakoo ambapo
ulipofika Kariakoo ilibidi Jeshi la Polisi liingilie kati ili kupunguza
foleni ya watu waliokuwa wakitaka kumshika mkono Diamond.
Diamond alipofika Buguruni aliamua kushuka kwenye gari ya wazi
aliyokuwa amepanda na kutembea kwa miguu na mashabiki wake mpaka
Kariakoo,hizi ni baadhi ya picha za mapokezi yake hayo.
PICHA NA MILLARDAYO
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi