MSANII MTUNISI AKIONA CHA MOTO MAHAKAMANI

Stori: Mayasa Mariwata na Chande Abdallah MSANII nyota wa filamu Bongo, Nice Mohammed  maarufu kama Mtunisi amekiona cha moto mahakamani baada ya kunyimwa dhamana na kutupwa mahabusu  katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Msanii nyota wa filamu Bongo, Nice Mohammed maarufu kama Mtunisi.

Mtunisi alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, ambapo baada ya kusomewa shtaka lake la kushambulia mwili, mtuhumiwa alikana na hivyo hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena.

Hata hivyo, Mtunisi alishindwa kupewa dhamana baada ya hakimu kutoridhishwa na afya ya mwanamke huyo, Aziz ambaye anaugulia nyumbani.

Katika hali nyingine, walinzi wa mahakama hiyo walionyesha mizengwe mikubwa kwa waandishi wa habari hizi, kwa kuwazuia kuingia ndani ya chumba cha mahakama wala kupiga picha, kwa madai kwamba sheria zao haziruhusu.

Wakionekana kama waliopewa maelekezo maalum, waliwataka kupeleka barua kutoka chombo chao cha kazi, kwani hata baada ya kuwakumbusha kuwa zoezi hilo lilishafanyika siku za nyuma, badala ya kupekua mafaili yao ili kuiona barua hiyo, waliwataka kwenda kuleta nakala ya barua iliyoandikwa awali, zoezi ambalo lilikuwa gumu kutokana na muda.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo