NJOMBE KINARA WA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KITAIFA



Ikiwa jana ni siku ya UKIMWI, Duniani ambapo Tanzania Kitaifa siku hiyo inafanyika Mkoani Njombe Juhudi za kupambana na maambukizi ya ukimwi mkoani humo zimezidi kushika kasi kutoka katika mashirika mbalimbali na kuanza kuungana na viongozi wa mila

Akizungumza na mwandishi wetu katika viwanja vya Sabasaba mkoani njombe, afisa uhusiano wa PSI kanda ya njanda za juu kusini, Sanday Beebwa amesema kuwa katika vitu vinavyo ongeza kasi ya maambukizi mkoani humo na Tanzania kwa ujumla ni pamoja na tamaduni na mila.
 
Beebwa amesema sasa wameanza kushirikiana na viongozi mbalimbali wa dini na viongozi wa kisiasa ambao wanawasihi kutoa elimu kwa wanachi wanapo kutana nao popote pale katika mikutani yao.
 
Aidha Beebwa ameongeza kuwa katika mikoa mitano ya juu Mikoa ya Nyanda ndio inaongoza huku mkoa wa njombe ukiwa ndio mkoa pekee Tanzania wenye tarakimu mbili za Kitakwimu katika Maambukizi
 
Maadhimisho haya  kilele chake ni jana ambapo mgeni rasmi alikuwa makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo