Balozi wa Yesu akiendelea kudhibitiwa na polisi |
Askari polisi akimthibiti balozi wa Yesu |
Balozi wa Yesu akithibitiwa wakati wa kampeni yake ya Injili Mtaa kwa Mtaa mjini Iringa leo |
Wananchi Iringa wakiwa wamelizunguka gari la Balozi wa Yesu leo |
Balozi wa Yesu akiwatuliza wafuasi wake |
Balozi wa Yesu akienda kupanda gari |
Balozi wa Yesu akiwa katika gari lake tayari kwenda Polisi kutii sheria bila Shuluti |
Gari la balozi wa Yesu likiondoka kwenda Polisi |
Balozi wa Yesu akizungumza baada ya kuachiwa na polisi |
Hii ndio CD ya Saluti ambayo leo balozi wa Yesu kajikuta akiwapiga kikweli kweli Saluti Polisi Iringa
MWIMBAJI
wa nyimbo za injili maarufu nchini Tanzania ambaye ni mlemavu wa
mkono mmoja Mwinjilisi Joseph Nyuki maarufu kwa jina la Balozi wa Yesu
amejikuta mikononi wa polisi wakati akiendesha harambee yake ya
Injili mtaa kwa Mtaa mjini Iringa.
Tukio
hilo la balozi wa Yesu kukamatwa na polisi limetokea leo majira ya
saa 8 mchana wakati gari la mwimbaji huyo wa Injili likipita katika
mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kueneza injili kwa kuuza CD
inayokwenda kwa jina la Saluti .
Mbali
ya kuwa na kibali cha Manispaa ya Iringa kinachompa uhuru wa
kueneeza injili kwa watu wote kupitia CD hiyo ya Saluti na kibali
hicho kupitishwa polisi bado askari polisi walimfuata balozi huyo
wa Yesu na kumtia nguvuni kuwa hapaswi kueneza injili kwa kupiga
kelele mitaani.
Askari
ambae jina lake halikuweza kunaswa mara moja alifika katika gari
lenye namba za Usajili T 364 DPD ambalo lilikuwa limefunga muziki
mnene na kupeperusha injili mtaani kiasi cha kila mmoja mjini hapa
kuvutiwa na vionjo vya mwimbaji huyo na kulifuata gari hilo kununua
CD kabla ya askari huyo kulipiga pini gari hilo eneo la Soko kuu
Miyomboni mjini Iringa .
Baada
ya kumsimamisha mwimbaji huyo kutoendelea na uuzaji wa CD hiyo
askari huyo alimtaka kuonyesha kibali pamoja na kuzima muziki na
kugeuza gari hilo kupeleka Polisi amri ambayo bila jeuri balozi wa
Yesu alitii huku akisema ndio kazi ya kueneza injili hiyo ambayo
kwake ameizoea .
Kwa
upande wao wananchi ambao walikuwa wakinunua CD wameeleza
kusikitishwa na hatua ya polisi kuzuia uenezaji wa injili huku kila
siku mji wa Iringa watu wanapita na magari wakitangaza Ma Disco na
matamasha yenye vichocheo vya maambukizi ya VVU huku wakiyafumbia
macho.
Mtandao
huu ulipofuatilia sakata hilo kituo cha polisi ulishuhudia
suala hilo likiishia nje ya kituo cha polisi baada ya askari huyo
kuyamaliza kiume na mwimbaji huyo nje ya kituo baada ya kuonyesha
kibali halali cha Manispaa ya Iringa na wakati askari huyo akihoji
zaidi juu ya kuzunguka kila kona likiwemo eneo hilo la polisi kwa
kupiga muziki ghalfa Mungu alionyesha nguvu zake kufuatia gari
jingine lililokuwa likiuza simu huku likipiga miziki ya duniani
likipita nje ya kituo cha polisi bila kukamatwa ndipo askari kwa
kuona hilo walimruhusu kuendelea na kazi ya kuitangaza injili.
Akizungumza
na mtandao huu mara baada ya kuachiwa huru Balozi wa Yesu alisema
kuwa polisi walifika na kumsimamisha na kumwomba kibali na baada ya
kuonyesha aliachiwa huru na kuwa polisi wametimiza wajibu wao na
kuwa hana kinyongo nao.
Pia
alisema kuwa ziara yake mkoani Iringa na mikoa mbali mbali ni
kuitangaza injili kupitia oparesheni yake ya Injili mtaa kwa Mtaa
kwa watu wote waokoke na kuwa anaifanya hivyo kama njia ya kuuza
CD yake baada ya kuchoshwa na unyonyaji unaofanywa na baadhi ya
studio kwa kuwalalia waimbaji wa nyimbo za Injili nchini.
via>>Matukiodaima
|