Hiki ndicho alichokiongea yule Msichana wa kazi (Hausigeli) aliyempiga Mtoto Uganda

Baada ya habari ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.

Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.

Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.

Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo