Akizungumza na waandishi wa habari jana Mjini Dodoma Mkurugenzi wa
Uchaguzi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Khalisti
Luanda alisema, katika matokeo hayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kimepata vijiji 1,248, chama cha TLP vijiji viwili, chama
cha NLD viwili, UDP vijiji vinne na chama cha CUF kilipata ushindi
katika vijiji 949.
Akitangaza matokeo ya Mitaa Khalisti alisema, Kati ya Mitaa 3,078
ilitoa matokeo , CCM imeshinda katika Mitaa 2,116,Chadema Mitaa 753,
CUF Mitaa 233,NCCR-Mageuzi Mitaa nane,TLP Mtaa mmoja,na ACT Mitaa tisa
Vyama vingine ni UMD, UDP na NRA kila kimoja kimeshinda Mtaa mmoja.
Khalisti alisema matokeo ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi Desemba yantarajiwa kutangazwa leo ambayo ni siku ya mwisho.
Aidha Mkurugenzi huyo aliitaja mikoa 11 ambayo imetekeleza
uchaguzi vizuri kuwa ni Arusha, Dodoma, Mbeya, Lindi, Mtwara, Ruvuma,
Katavi, kagera , Iringa na Njombe.
Na Mikoa ambayo uchaguzi haukufanyika kwa ufanisi ni Kigoma, Tabora, na Pwani.