Palikuwa na kituko cha mwaka
kilichotukia katika kituo cha polisi bulenga, wakati mwanamke mmoja
alipokuwa akiomba poo na huku akimtaka mumewe amsamehe na kumwachilia
aende zake kutokana na mumewe kuwa na hamu ya kufanya ngono isiyo na
koma.
Ruth Nakyeyune,alikuwa akilia na hanyamazishwi kwa madhila
apatayo kutoka kwa mumewe huku akimuomba mumewe mwenye asili ya Nigeria
bwana Sultan Ali Baba kwa pamoja ni wakaazi wa Nakuwade Bulenga,karibu
na barabara ya Mityana, mwanamke anaomba poo na mwenyekusema basi
yatosha na kutaka waachane kila mmoja ashike hamsini zake.
Bi
Nakyeyune amesema pia kwamba amekuwa si mvumilivu kwa muda mrefu na
asiyejali chochote na hataki kusikia jibu la hapana linapokuja suala la
ngono.bibi huyo amesema kwamba pindi anapokuwa hajisikii vizuri na
hawezi kufanya ngono,Sultan haelewi juu ya suala hilo,na
humnunia.sultani alipoulizwa juu ya kununa kwake alisema kwamba
hamuamini mkewe na sababu anazompa hivyo anadai anamdanganya na kumnyima
haki yake bure na kusema kuwa huwa hamridhishi,mara zote mwanamke huyoa
amekuwa akitafuta sababu na mara moja ameshawahi kumtishia atajiua.
Sultan
alimtaka mwanamke huyo amshukuru Muumba wake kwakuwa yeye ni mume mwema
asiyekunywa pombe kama wengine wafanyavyo,na kumshangaa mkewe
anashindwaje kumridhisha kirahisi?
Na kumuuliza mkewe bi
Nyakyeyune kwanini aliwaacha wazazi na jamaa zake kama hakuwa tayari
kumridhisha kingono,na kama shangazi zake ndo walomfunda na kumpeleka
kwake kwa shughuli za ndoa, vipi hayuko tayari?
Inaelezwa kuwa
wake wa awali wa bwana Sultan walimkimbia mwanamume huyo kwa tabia hiyo
hiyo ya kutoridhika kingono,lakini baadaye Sultani alimuomba mkewe
kusalia nyumbani kwa ajili ya watoto wao ili wawalee lakini mke alikataa
ushawishi huo.
CHANZO:BBC
