Mbunge huyo Millie
Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi
walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla
ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.
Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosoma katika mtandao wake wa facebook:
''Tulijaribu
kulemaza kikao hicho asubuhi yote.lakini ilipofika mwendo wa saa nane
waliwasili wakiwa wamejitayarisha ya kutosha.
Wabunge wengi
walipigwa.Mimi mwenyewe nilipigwa ngumi machoni na mbunge mmoja huku
wengine wawili wakijaribu kunivua nguo.lakini mimi si wa kulia lia
kwamba nimepigwa kofi! Mbunge aliyenipiga amejua kwamba mimi ni mbunge
wa Mbita aliyechaguliwa na wala si kuteuliwa.
Walipojaribu kunivua nguo
mimi mwenyewe niliwamalizia kuwavulia nguo.Mimi siogopi na nashkuru
nilivyoumbwa.
Sitakubali kutishwa kwa kutumia jinsia yangu'',aliandika bi
Millie..
Maandishi haya baadaye yalifuatiwa na mengine yaliosema kuwa ameenda kupigwa picha na kuangaliwa jicho lake hospitali.
VIA BBC