LADY JAY DEE ADAI HANA MPANGO WA KUJIINGIZA KWENYE SIASA


MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' amesema kamwe hatarajii kujiingiza katika masula ya siasa kama wanavyofanya wanamuziki wenzake.
 
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo Dar es Salaam jana, baada ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti hilo katika Jengo la Hifadhi House katika makutano ya Barabara za Azikiwe na Samora.
 
"Binafsi sitarajii kuingia katika masula ya siasa mimi nitaendelea na muziki na hao wenzangu waliojiingiza katika siasa ni utashi wao."
 
Alisema anafurahi kufanya muziki na wala hajuti kwa kuwa unamuongezea kipato,kikubwa ni kutunga nyimbo zenye maudhui na mvuto na kwa wakati husika.
 
Baadhi ya wanamuziki waliojiingiza katika siasa ni Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule 'Profesa J, Khadija Shabani 'Keisha' Ummy Wenslaus 'Dokii, na wengine kama Fullgence 'Mwanacotide' ambaye yupo Chadema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo