Koletha: Sipendi Uhusiano Na Wasanii

Koletha: Sipendi Uhusiano Na Wasanii
Mrembo na mwigizaji  wa filamu  hapa Bongo, Coletha Raymond ‘Koletha’ amefunguka kwamba tangu aingie kwenye fani hiyo hajawahi kuwa na mpenzi msanii na hapendi hata kuwasikia.

Akipiga stori na mwandishi, Koletha alisema kutokana na kwamba anazijua tabia zao kwani anafanya nao kazi pia wakati alipoanza fani hiyo alijiapiza kwamba hatakuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu anayefanya naye kazi.

“Sijawahi kutoka na msanii na siwezi kutoka nao kimapenzi kwa sababu ni kitu ambacho nimejiapiza halafu pia inapunguza ufanisi wa kazi hivyo sina hata wazo la kuwa nao kwa kweli, mimi huwa nakuwa na uhusiano na watu wa kawaida,” alisema Koletha.
GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo