HALIMA MDEE NA WENZAKE WAPANDISHWA TENA MAHAKAMA YA KISUTU

 
MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (35) na wenzake wanne walisomewa maelezo ya awali jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo walikubali kuwa wafuasi wa Chadema na kwamba wanafahamiana.

Mbali na Mdee washitakiwa wengine ni Rose Moshi (45), Renina Peter, Anna Linjewile (48), Mwanne Kassim (32), Sophia Fanuel (28), Edward Julius (25) Martha Mtiko (27) na Beaty Mmari (35).

Wakisoma maelezo hayo, Mawakili wa Serikali Ahmed Salim na Wakili Mwandamizi Tumaini Kweka walidai mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda, kwamba washitakiwa hao walikamatwa kwa katika Mtaa wa Ufipa wakiwa wamebeba mabango na kukana mashitaka yote.

Pia walidai kwamba washitakiwa hao walikaidi amri halali ya Polisi iliyowataka kutawanyika baada ya wafuasi hao kutaka kutembea kwenda Ofisi ya Rais.

Salim alidai baada ya wafuasi hao kukaidi kufuata amri hiyo, polisi walitumia nguvu kuwatawanya kwa kosa la kufanya fujo.
Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala aliiomba mahakama hiyo kufuta shitaka la pili kwamba washitakiwa hao kwa pamoja walikusanyika kwa lengo la kutembea kwenye Ofisi ya Rais kwamba shitaka hilo lina mapungufu kisheria, kwani halikutaja vifungu vya kisheria.
Hata hivyo, upande wa mashitaka ulidai kwamba hakuna madhara yoyote endapo vifungu hivyo havitatajwa. Kesi itatolewa uamuzi Januari 5 mwakani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo