Hiace
yenye namba za usajili T761 CKD ikiwa imepinduka baada kuparamia tuta
la barabarani na kupoteza mwelekeo kisha kutumbukia mtaroni katika eneo
la Buhangija mjini Shinyanga barabara ya Tinde-Shinyanga leo saa nne na
nusu asubuhi.
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga limesema waliofariki dunia katika ajali ya
Hiace yenye namba za usajili T761 CKD iliyotokea le asubuhi mjini
Shinyanga ni 9,majeruhi 9.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwamu amewataja waliofariki dunia kuwa ni Nkingwa
Kariagi(50) mkazi wa Mwamanota Kishapu,Kelvin Michael(21) utingo wa
gari hilo,mkazi wa Ngokolo,mjini Shinyanga na Masanilo Jisandu(miaka 50)
mkazi wa Negezi Kalitu Kishapu.
Wengine waliofariki duni ni Amina Abdallah,mkazi wa Mbika Kahama,Nkola Shija(20) mkazi wa Kahama,Elizabeth Ngusa (15) mkazi wa Maswa na wengine watatu hawajajulikana majina,umri,kabila wala makazi yao.
Wengine waliofariki duni ni Amina Abdallah,mkazi wa Mbika Kahama,Nkola Shija(20) mkazi wa Kahama,Elizabeth Ngusa (15) mkazi wa Maswa na wengine watatu hawajajulikana majina,umri,kabila wala makazi yao.
Majeruhi katika ajali hiyo ni 9,ambao ni Peter
Yustasi(49) mkazi wa Sengerema,Frola Ngudungi(35) mkazi wa Ushetu
Kahama,Yesaya Samwel(40) mkazi wa Singida,Kwimba Damayake(36) mkazi wa
Iramba Tabora na Nyanzobe Henge(70) mkazi wa Uloa Kahama.
Majeruhi wengine ni Katumbi Nangi(36) mkazi wa Uloa Kahama,Emmanuel John(22) mkazi wa Mwakitolyo,Jimoda Kaliagi(52) mkazi wa Mwamanota Kishapu na Kalwa Mwandu(36) mkazi wa Kahama.