Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner.
Kwenye
mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa
akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner
lakini alisema alikuwa akiteswa.
Kabla
ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote amekuwa
akiepuka kuongea masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.“Kitu
kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye huwa
napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti au
wapi,” alisema.
“Na
ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye
maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote
wanachohisi, chochote wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu
anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na waendelee kuliheshimu
hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na privacy.
Ingekuwa
kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza kuelezea mambo yake, mama
yake jana walishinda njaa, au mume wake alimfanya hivi, sidhani kama
kuna mtu yeyote anapenda kuelezea maisha yake, hata matatizo yake mbele
za watu.”
“Kwahiyo mpenzi wako Gadner bado mko naye,” aliuliza mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho na mchekeshaji, MC Pilipili.
“Swali nafikiri hujalijibu, umemtosa, hujamtosa?,” aliuliza Fadhil Haule, mtangazaji mwingine wa show hiyo.
“Nimemuacha,” alijibu Jide. “Huyu (Gadner) tumeshamalizana.”
Isikilize interview hiyo hapo chini.