Katika kipindi cha maswali na majibu leo Novemba 24, Mbunge Rajabu Mbarouk Mohammed aliuliza swali; “..Suala
la usalama wa Wabunge ni pamoja na maeneo wanayofanyia kazi lakini vile
vile na maeneo ambayo wanayoishi wabunge, Mheshimiwa Spika tangu kuanza
kwa sakata la ESCROW hali imekuwa tete kwa Usalama wa Wabunge, nini
tamko la Serikali juu ya ulinzi na usalama wa Wabunge katika maeneo ya
kazi lakini vile vile katika maeneo wanayoishi?..”
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Januari Makamba alijibu;”…Serikali
inafanya tathimini wakati wote ya matishio ya usalama wa Nchi lakini
usalama wa viongozi ikiwemo Wabunge na inachukua hatua muafaka
kuhakikisha kuwa viongozi wao wako salama, kwa hiyo Serikali inapenda
kuwahakikishia Wabunge kwamba licha ya yote yanayoendelea usalama wao
uko salama na wasiwe na wasiwasi watimize majukumu yao kama
inavyohitajika…”
Naye Spika wa Bunge Anne Makinda alisema kuhusu mpango ambao Serikali inao kuhusu usalama wa Makazi ya Wabunge; “…Tunakusudia kujenga eneo la Vijiji vya Wabunge ambapo wanaweza kulindwa kwa pamoja kuliko ilivyo sasa kila kitu ni mipango…”