Wakiongea na kituo cha ITV mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema ; “…
Majira ya saa nne kasoro Mwalimu alikuja kunipa taarifa kwamba kuna
ajali imetokea baada ya kufika eneo la tukio nikaambiwa kwamba
Mwanafunzi aliyeangukiwa na mti na amefariki hapo hapo na wasamaria
walisaidia kumtoa katika hilo gogo alilokuwa ameangukiwa lakini nilikuta
alikuwa kashatolewa pale kwenye eneo na amefunikwa…”
Shuhuda mwingine wa tukio hilo amesema “…Ni
msiba mkubwa ambao umetukuta ni mpango wa Mungu, lakini pamoja na
mpango wa Mungu naweza ukaona mazingira ya Shule yalivyo kuna vichaka
hivi vichaka kuna mikorosho iliyoanguka, haikuanguka moja kwa moja
imebaki nusu kamati za shule zipo, ilikua kazi za kamati ya shule ili
kumalizia hiyo miti na mazingira ya Shule yakafyekwa kukawa kuzuri,
sababu licha ya hiyo miti kuna nyoka, kuna watu amabao hawana nia nzuri
wanaweza kukaa na wakachukua watoto, lakini kamati ya Shule imekaa kimya
na wapo Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe wake wito wangu mimi ni kwamba
ikiwezekana kamati ya Shule wajipime waone kama inawezekana waachie
ngazi...”
Naye kiongozi wa kamati ya Mazingira shuleni hapo amesema; “…
Tutatafuta watu ambao wanakatakata mkaa ili tukae nao pamoja waanze
kuipunguza kwa sababu tumeshaiona hatarishi kipindi kirefu kwa hiyo
tushaamua suala hilo nafikiri baada ya muda fulani tutanza
kulishughulikia…”
Kuisikiliza taarifa niliyoirekodi wakati kituo cha ITV kikirusha taarifa hiyo bonyeza play hapa.