Utupaji watoto wachanga katika mto Ngarenaro Mkoani Arusha umekithiri
hali inayohatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo ambayo hutumia maji
ya mto huo kwa shughuli zao za kila siku.
Kutokana na hilo wakazi wa eneo hilo hulazimika kufanya usafi mara
kwa mara na kulalamikia kukuta miili ya vichanga ambayo hutupwa maeneo
hayo kila wakati.
Baadhi ya wakazi hao walisema mto huo ambao chanzo chake kinatoka
katika Mlima Meru ni muhimu kwao kutokana na maji yake kutumika kwa
matumizi ya nyumbani na hata umwagiliaji wa mboga mboga.
“Unaweza kwenda kuteka maji ukakutana na mabaki ya miili ya watoto
huku wengine wakitupa taka kwa kukwepa kulipa ushuru wa takataka ambao
ni shilingi 1,000 kwa Halmashauri ya jiji.