Kumekuwa
na taarifa katika vyombo vya habari na mitandaoni pia kwamba Serikali
ilikuwa na mpango wa kuiondoa Jamii ya Wamasai katika eneo la Loliondo,
ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu aliwahi kukanusha
juu ya hilo siku tatu zilizopita.
Jana kupitia ukurasa wa Twitter, Rais Kikwete
ameandika kwamba Serikali haina mpango na wala haitowatoa Wamasai kutoka
katika ardhi hiyo ambayo ni urithi wa mababu wa jamii hiyo.
Ujumbe aliouandika Rais kupitia ukurasa wake wa Twitter jana Novemba 23 unasomeka hivi; “…There has never been, nor will there ever be any plan by the Government of #Tanzania to evict the #Maasai people from their ancestral land…“– @jmkikwete
Katika taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari ilisemekana
kuwa lengo la kuiondoa Jamii hiyo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za
mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.