Tumezoea Wabunge wetu wakipewa nafasi ya kuchangia jambo ndani ya kikao cha Bunge huwa wanaanza kwa pongezi, utasikia hivi; “.. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge au Waziri………”
Jumatatu kikao cha Bunge kitaendelea na nadhani hautoshtuka ikitokea Mbunge hata mmoja akisema hivi; “… Nimpongeze sana Mheshimiwa David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kufunga ndoa siku ya Jumamosi..”
Yes.. ni kweli.. mbunge huyo amefunga
ndoa November 22 2014 Kigoma, ujumbe alioandika Zitto Kabwe kwenye
ukurasa wake wa Facebook ni huu hapa; “..Bwana Harusi David Kafulila akiwa na msimamizi wa ndoa yake Deo Filikunjombe na marafiki zake David Silinde na Mwami..” halafu kuna picha aliyoiweka akiwa na Wabunge hao.