Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani,Nurdin Babu ameagiza
wanafunzi24 wa Sekondari mbalimbali Wilayani humo waliopata ujauzito
kuripoti kituo cha polisi November25 mwaka huu ili wasaidie kutoa
ushirikiano wa kuwakamata wahusika waliowapa mimba na kuweze kukamatwa.
Sambamba na wanafunzi hao pia wazazi au walezi wa wanafunzi hao
wametakiwa kuripoti wakiwa na watoto wao ambapo atazungumza na wazazi
pamoja na wanafunzi hao ili kujua tatizo ni nini.
Babu alisema taarifa za watoto 26 walipata ujauzito katika kipindi cha
Januari hadi Oktoba si nzuri na lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe
ili kuondokana na matatizo hayo ndani ya jamii.
Alisema idadi ya wanafunzi waliokatishiwa masomo ni kubwa na Serikali haiwezi kulifumbia macho suala hilo.