Wauguzi wa Hospitali ya Bugando wakiendelea kuchangisha fedha kwa
ajili ya kupatikana lishe kwa watoto mapacha watatu ambao wamempoteza
mama yao,shangazi wa watoto hao ametoroka na fedha za misaada
zilizotolewa na wasamaria wema.
Mapacha hao walizaliwa katika hospitali ya Misungwi wakiwa ni watoto
watatu walionusurika kati ya watano waliozaliwa ambapo mama yao
alifariki muda mfupi baada ya kujifungua pamoja na watoto wengine
wawili.
Kutokana na tukio hilo wauguzi wamesitisha kuomba misaada kupitia
namba ya simu iliyotolewa badala yake wafike hospitali na kuikabidhi kwa
bibi anaewalea.
Zaidi ya shilingi laki mbili zilichangwa kupitia simu hiyo lakini
hazikuweza kutumika baada ya shangazi yao huyo kutoweka nazo akidai
anakwenda kuzitoa kwa wakala.