Ni miezi sita sasa baada ya
wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka wanafunzi
wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria, wasichana watatu
ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya
Kihausa ya BBC.
Tukio hili linakuja wakati serikali ya Nigeria
ikiwa katika makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram
hatua itakayo saidia kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi hilo
.
'' nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu
aliponikamata kwa nyuma na kusema watakupiga risasi kama utafanya hivyo.
Nikasema, nini utofauti wataniua mimi hapa na kuacha maiti yangu
ikusachukuliwa nilikuwa nalia na kuomba mpaka tulipoifikia kambini"
Anasimulia msichana mmoja alitoroka mikononi mwa Boko Haram
Akizungumza
katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC, Msichana huyu
anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wanapinaji wa Boko
Haramu walipomteka yeye na wasichana wengine.
Zaidi ya wasichana
200 kati miongoni mwao walikuwa walitekwa lakini wale waliokimbia
walibahatika kutoingia katika hofu kubwa kwenye mikono ya watekaji.
Shirika
la kimataifa la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch limesema
wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haramu wamekuwa wakinyanyaswa,
kubakwa na hata kulazimishwa kuolewa.
Katika ripoti mpya ya
shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam wamewawateka wanawake
Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.
Serikali ya Nigeria
hivi karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya
Boko Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia huru
wasichana wa hao waliotekwa huko Chibok.
Lakini Boko Haram wenyewe
hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano na
hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana haohivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua..
bbc