TSD YATOA MAJIBU YA MALALAMIKO YA WALIMU MKOANI NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya NJOMBE

Idara ya  Utumishi wa  Umma Kwa Walimu TSD Mkoa wa Njombe Imewataka Walimu Kuacha Tabia ya Kulalamika Kwa Kila Jambo Bila Kufahamu Taratibu Zake Jambo Ambalo Huleta Taswira Mbaya Kwa Jamii.

Kauli Hiyo Imetolewa na Katibu wa Idara ya Utumishi wa Walimu Mkoa wa Njombe Mwalimu Letisia Mwayeya Wakati Akizungumza na Uplands Fm Ofisini Kwake Kufuatia Kuwepo Kwa Baadhi ya Malalamiko Juu ya Kucheleweshwa Kupandishwa Vyeo Kwa Baadhi ya Walimu.

Bi.Mwayeya Amesema Kuwa Baadhi ya Walimu Wamekuwa Wakilalamikia Suala la Kuchelewa Kupandishwa Vyeo Pindi Wanapovuka Ngazi Moja Kwenda Nyingine Jambo Ambalo Hufanyika Kwa Kuzingatia Taratibu za Utumishi wa Umma.

Aidha Amesema Kuwa Kama TSD Imekuwa Ikiendelea Kushughulikia Malalamiko Hayo Siku Hadi Siku Kwa Kutoa Elimu Pindi Yanapotokea Malalamiko Kama Hayo Bila Kujua Taratibu Zake.

Katika Hatua Nyingine Amesema Miongoni Mwa
Sababu Zinazochangia Kuchelewa Kupandishwa Vyeo Kwa Baadhi ya Walimu ni Pamoja na Utovu wa Nidhamu Kama Utoro Ikiwemo Kuchelewa Kwa Fedha Kwa ajili ya Kukaa Vikao Vyenye Maamuzi ya Kupitisha Walimu Wanaohusika Kupanda Madaraja.

Sanjari na Hayo Lakini Pia Ametaja Hatua za Kufikia Kupanda Kwa Vyeo Kwa Walimu Hao Kuwa ni Kwa Walimu Wote Waliofanyakazi Kwa Muda wa Miaka Mitatu Baada Ajira Au Kujiendeleza Kimasomo.

Hivi Karibuni Chama Cha Walimu Tanzania CWT Kilitoa Siku 14 Kwa Serikali Kuhakikisha Imewapandishwa Vyeo Walimu Wote Wanaostahili Kabla ya Kufanya Maandamano ya Nchi Nzima Kwenda Kwa Wakurugenzi Kudai Haki Hiyo Jambo Ambalo Limeonekana Kuwa Changamoto Kubwa Kwa Serikali Katika Sekta ya Elimu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo