Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, amewatoa hofu
wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule za Msingi Temboni, Malamba
Mawili na Saranga, jijini Dar es Salaam kuwa hakuna tukio la utekaji
watoto lililotokea.
Alisema hadi sasa hakuna mzazi aliyetoa malalamiko polisi kuhusu tukio la watoto kutekwa na kuwaonya watu wanaotoa taarifa zinazoleta hofu katika jamii, kuacha tabia hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
“Unajua huo ulianza Kawe na sasa umehamia Kimara. Hakuna taarifa yoyote ya kutekwa wanafunzi kwa kutumia pikipiki wala Noah nyeusi. Huo ni uvumi tu,” alisema Kamanda Wambura.
Alisema uvumi huo unawatia hofu wanafunzi na hivyo kuwafanya washindwe kwenda shule kujifunza kwa kuogopa uvumi wa kutekwa na kwa hiyo, Serikali haiwezi kuvumilia.
Uvumi huo ulizuka juzi majira ya saa 7:00 mchana baada ya wazazi na walezi wa wanafunzi, kutarifiwa na walimu kufika shuleni katika shule hizo kuwachukua watoto wao.
Ilidaiwa kuwa wanafunzi hao walitoroshwa na watu wasiofahamika kwa kutumia gari aina ya Noah lenye rangi nyeusi, ambalo ilifika katika shule hiyo.