Chama cha Demokrasia na maendeleo
Chadema kimewataka watanzania kujiwekea utaratibu wa kuisoma katiba
inayopendekezwa ili kuelewa yaliyondani ya katiba hiyo kwa lengo la
kugundua mazuri na mabaya yaliyo ndani ya katiba hiyo pendekezwa badala
ya kutegemea kusikia kutoka kwa wanasiasa ambao wanaweza kuwadanganya
kwa lengo la kulinda maslahi yao ya kisiasa.
Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalimu ametoa wito huo
wakati akiwahutubia wakazi wa tarafa ya idodi mkoani Iringa ambapo
amesema katiba hiyo inayopendekezwa ina mapungufu mengi na imetungwa kwa
kuzingatia maslahi ya kundi fulani la wanasiasa ambapo licha ya
kuwanyima wananchi nguvu ya kuiwajibisha serikali pia imeliondolea meno
hata bunge la jamhuri kuisimamia serikali.
Kwa upande wake mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
amewataka wabunge wa mkoa wa Iringa kuunga mkono juhudi zake za kuitaka
serikali kuujenga uwanja wa ndege wa nduli mkoani Iringa katika kiwango
cha kimataifa ili kusaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea
hifadhi ya taifa ya ruaha ambayo ndiyo ya pili kwa ukubwa barani afrika
lakini ikiwa nyuma kimapato kulinganisha na hifadhi nyingine za ukanda
wa kaskazini.
Naye mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa Mustapha Msowela
amewataka wananchi kujiandikisha katika daftarai la makazi na lile la
kudumu la wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wanye nia ya
kuwatumikia katika chaguzi zijazo huku makamu mwenyekiti wa baraza la
vijana la chama hicho Patrick Sosopi akiwataka wananchi hao kutochagua
viongozi wanaotokana na rushwa kwenye vyama vyao.