Ziara ya mwenyekiti wa baraza la
wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee
imepata mapokezi makubwa jijini Mwanza ambapo amewataka wananchi wa jiji
la Mwanza wasikubali kulazimishwa kuikubali katiba inayopendekezwa
kwani haikuzingatia maoni ya wanachi ya kutaka uwazi katika rasilimali
za nchi zilizopo zitumike kunufaisha wananchi badala yake katiba hiyo
inawapa mamlaka vigogo kuendelea kunufaika na rasilimali za taifa huku
wananchi wakiendelea kuumia.
Mdee ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano
wa hadhara katika uwanja wa Frahisha jijini Mwanza ambapo amesema
Chadema hawatakubali kupigia kura ya ndiyo rasimu ya katiba
inayopendekezwa kwani wananchi wakipendekeza katiba mpya iweke wazi
mikataba inagusa maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha mikataba anayoingia
rais inakuwa wazi katika magazeti ya serikali ili wananchi wajue
watakavyonufaika na mikataba hiyo lakini katiba inayopendekezwa
imetupilia mbali maoni hayo ambapo amesema katika hiyo imejaa
mapendekezo ya kulinda maslahi ya wachache na sio wananchi masikini
walio wengi.
Naye naibu katibu Bawacha taifa Kunti Yusuph na katibu wa vijana
taifa Edward Simbeye wamewataka wananchi wa jiji la Mwanza kutokubali
kuburuzwa kuipigia kura ya ndiyo rasimu ya katiba inayopendekezwa na
badala yake waisome kwa umakini na wahakikishe wanachagua viongozi
wanaofaa katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku vijana wakitakiwa
kuacha kushabikia watu wanaowalazimisha watanzania kupiga kura ya ndiyo
katika rasimu inayopendekezwa.