Msanii
wa muziki wa asili Tanzania ambaye pia ni msanii wa maigizo na filamu,
Mrisho Mpoto akizungumza jambo mbele ya waaandishi wa habari na wamiliki
wa blogs mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao ya
kijamii. Mrisho alisimama kuzungumza dakika chache baada ya wimbo
alioimba na Banana Zoro kuzinduliwa, unaojulikana kama 'Futa, Delete
Kabisa'. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA),John Nkomo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkomo,
akizungumza mbele ya wamiliki wa blogs mbalimbali Tanzania, waandishi wa
habari katika warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao
ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha suala zima la maendeleo.
Prof.Nkomo amesema kuwa kwa sasa kumekuwepo na ongezeko kubwa la matumizi ya intaneti kwa Watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni.Amesema kuwa wengin wa watumiaji wa Intaneti,matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandano ya kijamii kama vile facebook,Twitter,BBM,Linkedin na Blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikwemo za kimaendeleo,burudani pamoja na michezo.

Baadhi
ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), waandishi
mbalimbali wa habari pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii, Blogs,
wakisikiliza maneno mazuri kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Tanzania,
Profesa John Nkomo, hayupo pichani. Hii ni sehemu maalumu ya kuonyesha
kuwa TCRA wanatambua mchango wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na
wamiliki wao kwa ujumla.
Meneja
Uhusiano wa TCRA,Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali wa
mambo ya habari za kwenye mitandao,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya
kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano,Warsha hiyo
imefanyika leo Makao makuu ya Ofisi hizo,zilizopo barabara ya Sam Nujoma
jijini Dar.
Wadau
wa mawasiliano wa mitandao ya kijamii, blogs, wakisikiliza hoja
mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
TCRA katika uzinduzi wao wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya
kuhamasisha maendeleo ya Taifa.